Ligi Kuu Tanzania bara kubakia na timu 16

58

Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPBL) imekusudia kupunguza idadi ya timu zitakazoshiriki katika ligi kuu Tanzania bara kutoka timu 20 hadi 16 kwa misimu miwili ijayo, 2022/23.

Baada ya kufanyika kwa tathmini ya Ligi Kuu nchini Tanzania msimu uliopita, tumeamua kufanya mabadiliko madogo kuanzia Ligi Kuu na Ligi nyingine ndogo.

Akizungumza na Wanahabari wa michezo nchini Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema wamekutana na makocha na viongozi wa vilabu na kufanya majadiliano, wameamua kufanya marekebisho katika uendeshaji wa ligi hiyo ikiwa ni pamoja na kupunguza idadi ya timu.

Aidha, Boniphace Wambura, amethibitisha idadi ya wachezaji wa kigeni wanaopaswa kusajiliwa na timu za Ligi Kuu watabaki kuwa kumi kama ilivyokua msimu uliomalizika uliopita 2018-19.

“Kuhusu wachezaji wa kigeni, tutaendelea na wale wale 10, ila sharti wawe wenye vigezo tunavyovihitaji sisi TFF,” alisema Wambura na kuvitaja vigezo hivyo kua ni pamoja na mchezaji anayesajiliwa na timu ya ligi kuu anapaswa kuwa anacheza timu ya taifa analotoka iwe timu ya vijana au ya wakubwa.

Kigezo kingine ni mchezaji huyo awe ametoka timu inayoshiliki Ligi Kuu ya nchi aliyotoka ama daraja la kwanza.

Mtendaji huyo alisema wachezaji wote wa kigeni watathibitishwa na TFF ili kuzitumikia timu zao na ambao watakosa vigezo hawataruhusiwa kucheza mchezo wowote.

Author: Bruce Amani