Ligi kuu nchini Ubeligiji maarufu kama Belgian Pro imefutwa rasmi leo Alhamis Aprili 2 na kuwa taifa la kwanza kufuta ligi zake kutokana na hofu ya virusi vya Corona.
Tofauti na inavyoelezwa katika nchi nyingine ndani ya bara la Ulaya, Ubelgiji wameamua kuipa Club Bruges ubingwa wa ligi wakitumia mfumo wa kinara katika msimamo kutwaa taji hilo.
Ligi hiyo ilikuwa imebakiza mchezo mmoja kumalizika kipindi inasimamishwa lakini kama mtindo wao wa kucheza ligi hufuata hatua ya mtoano (play-offs) kuamua klabu itakayokamata nafasi ya kwanza.
Wakurugenzi wa ligi wamefikia maamuzi hayo kisha kupeleka mapendekezo kwenye mkutano mkuu licha ya maamuzi hayo kupitishwa.
Aprili 15 ndipo watatoa taarifa rasmi juu ya kufutwa kwa ligi lakini pia ndiyo siku itatumika kuamua vilabu vya kupanda na kushuka daraja. Club Brugge wanaongoza ligi kwa tofauti ya alama 15 kwa timu iliyo nafasi ya pili Gent.
“Kama bodi ya wakurugenzi tumeamua kusitisha ligi kutokana na kutokuwepo kwa uwezekano wa kuendelea na mashindano baada ya Juni 30,” ilisema taarifa hiyo.