Ligi ya Mabingwa yarudi, Liverpool, Barcelona dimbani

52
Ligi ya Mabingwa Ulaya inarejea tena leo Jumanne usiku kwa kushuhudia miamba mbalimbali kutoka kwenye mataifa ya bara la Ulaya yakipepetana vilivyo.
Wakati michuano hii pazia lake likifunguliwa leo kuna maswali muhimu ya kujiuliza.
Je, Liverpool inaweza kufuata nyanyo za Real Madrid kunyakua taji mara tatu mfululizo, inawezekana kuingia kwa Antonio Griezmann kukaleta uhai ndani ya FC Barcelona, Manchester City chini ya Pep Guardiola ametawala soka la England nguvu hiyo itafanya msimu wa huu kunyanyuka taji la Uefa ambalo Pep alibeba mara ya mwisho akiwa Catalan.
PSG haifahamika kama imejiandaa au vp, Juventus na Ronaldo bado wanajipanga ili muda uwepo wa matazamio?.
Hayo ni baadhi ya maswali ya kujibu kupitia muda.
Maswali haya yapatapo tiba ndiyo kuanza kwa michuano yenyewe.
Septemba 17, yaani leo Jumanne Michezo minne itapigwa hatua ya makundi ambapo  Fc Barcelona wamesafiri kuifuata Borrusia Dortmund, Liverpool itamenyana dhidi ya Napoli, mabingwa wa Europa Ligi Chelsea watacheza na Valencia ya Hispania.
Siku ya Jumatano kutakuwa na muendelezo wa mashindano hayo ambayo yatafikia tamati mwezi Mei, mechi ya siku itakuwa kati ya Paris Saint Germain dhidi ya Real Madrid, Juventus wanarejea tena Wanda Metropolitano
Yote kwa yote wachambuzi wa soka wamekuwa wakizitaji klabu nne kama zenye uwezekano wa kutwaa taji la Uefa zaidi ya nyingine. Mabingwa Liverpool hutajwa kama hatari zaidi, wakati Barcelona, Manchester City na Juventus ni miongoni mwanzo.
Utabiri wako umekaaje kuhusu ubingwa wa msimu, Nani kutwaa taji hili?

Author: Asifiwe Mbembela