Liverpool, Chelsea zapagawa, Barcelona ngoma droo

Liverpool imeangukia pua ugenini katika dimba la Napoli baada ya kukubali kipigo cha goli 2-0 katika mchezo wa kwanza wa kwenye makundi wa msimu mpya wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Liverpool ambayo ni mabingwa watetezi wa taji la Uefa wamejikuta wako nyuma baada ya magoli ya haraka ya Napoli kipindi cha pili kupitia kwa Dries Mertnes kwa njia ya penati na Fernando Llorente aliyetumia makosa ya mlinzi Virjin.

Mechi nyingine, Chelsea imeanza kampeni ya kuwania taji hili kwa kipigo cha goli 1-0 dhidi ya Valencia ya Hispania. The Blues watajilaumu wenyewe baada ya kukosa penati dakika za lala salama kupitia kwa Ross Backley.

Mechi ya siku, Borrusia Dortmund dhidi ya Fc Barcelona imetamatika kwa suluhu ukiwa pia ni mchezo wa awali, mshambuliaji Marcus Reus amekosa penati kwenye mechi hii.

KRC Genk yaangukia kipigo kizito kutoka kwa Waaustria Slavia Plague cha goli 6-2.

Inter Milan wamecheza katika dimba la nyumbani wameshindwa kuutumia vizuri kwa kulazimisha sare ya goli 1-1 dhidi ya Slavia Plague katika mchezo uliopigwa majira ya jioni masaa ya Afrika Mashariki.

Kesho Jumatano kutakuwa na michezo miwili ya kukatana nashoka kati ya mabingwa wa hivi karibuni mara tatu mfululizo Real Madrid dhidi ya PSG na Atletico Madrid watakuwa wenyeji wa Juventus ya Italia.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends