Liverpool matatani baada ya kichapo cha PSG

Borussia Dortmund, Atletico Madrid, Schalke na Porto zote zimefuzu katika hatua ya 16 za mwisho ya Ligi ya Klabu bingwa Ulaya katika mechi zilizochezwa jana usiku. Dortmund ilipata tiketi yake ya hatua ya mtoano baada ya kutoka sare tasa nyumbani dhidi ya Club Brugge. Atletico iliizaba Monaco 2-0 kufuatia mabao ya kipindi cha kwanza kutoka kwa Antoine Griezmann na Koke.

Porto na Schalke zilitinga kutoka Kundi D kabla ya timu hiyo ya Ureno kuwalaza wageni wao kutoka Ujerumani 3-1 kwa sababu Galatasaray ilipigwa 2-0 na Lokomotiv Moscow katika mechi ya mapema. Barcelona ilikamata nafasi ya kwanza ya Kundi B kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya PSV Eindhoven.

Tottenham iliifunga Inter 1-0 na sasa katika mechi zijazo, za Desemba 10, Spurs lazima watoshane na matokeo ya Inter Milan ili kupata nafasi ya pili kutoka Kundi B lakini watacheza dhidi ya Barcelona na Inter wacheze na PSV Eindhoven.

Katika Kundi C, Napoli, Paris Saint Germain na Liverpool zinaweza zikafuzu. Liverpool wanapaswa kuwazaba Napoli 1-0 au mabao mawili bila jibu nayo PSG ipate tu pointi moja dhidi ya Red Star Belgrade. Shakhtar Donetsk na lyon zitakwaruzana lakini Shakhtar watahitaji kuwashinda Lyon ili kupata tiketi ya mwisho kutoka Kundi F.

Mabingwa watetezi Real Madrid, Manchester City, Bayern Munich na Juventus tayari zimefuzu. Manchester United, Roma na Ajax pia zilitinga hatua ya mtoano.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends