Liverpool ndio mabingwa wapya wa Ulaya

46

Liverpool wamebeba kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya sita baada ya kuilaza Tottenham katika mechi iliozileta pamoja timu mbili za England katika fainali ya mjini Madrid.

Mohamed Salah alifunga goli la penalti baada ya dakika mbili kufuatia makosa ya Moussa Sissoko aliyenawa mpira uliopigwa na Sadio Mane katika eneo hatari

Baada ya penalti hiyo, kipindi kilichosalia cha mchezo hakikuwavutia wengi kutoka timu zote mbili hadi pale Divock Origi aliyefunga magoli mawili katika nusu-fainali dhidi ya Barcelona alipoifungia Liverpool goli lao la pili.

Hata hivyo kiwango cha mchezo hakitamjalisha mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp ambaye alipoteza fainali ya kombe hilo mwaka uliopita dhidi ya Real Madrid.

Hatua ya Tottenham kumuanzisha mshambuliaji Harry Kane ambaye alikuwa akiuguza jeraha kwa kipindi cha miezi miwili haikuzaa matunda.

Spurs ambao hawakupata fursa ya kufanya shambulizi lolote katika lango la Liverpool hadi dakika ya 73 walipata fursa nzuri ikiwa imesalia dakika 10 wakati Son Heung -min na Lucas Moura aliyeingia katika kiupindi cha pili waliposhambulia lakini kipa Allison alkapangua makombora yao.

Ni kombe la kwanza la Liverpool chini ya ukufunzi wa Klopp, ambaye alikuwa amepoteza fainali sita ikiwemo fainali mbili za kombe la mabingwa Ulaya.

 

Author: Bruce Amani