Liverpool wawacharaza Porto na kuweka miadi na Barca

53

Weka kando kwanza habari za kukutana na Lionel Messi na timu yake ya Barcelona. Kwa sasa wanastahili kusherehekea mafanikio yao kabla ya kuanza kuyanoa makali na kuweka mkakati mahsusi wa kumdhibiti Lionel Messi. Liverpool iliikanga Porto kwa kuibamiza jumla ya mabao 6-1 na katika mikondo miwili ya robo fainali na kutinga nusu fainali ya Champions League.

Huku wakiwa kifua mbele 2 – 0 kutokana na mechi ya mkondo wa kwanza uwanjani Anfield, mabao kutoka kwa Sadio Mane, Mohammed Salah, Roberto Firmino na Virgil van Dijk yalidhihirisha kazi mufti kabisa aliyofanya kocha Jurgen Klopp katika mechi hiyo.

The Reds walilizimika kustahimili kishindo cha mashambulizi ya mfululizo katika dakika za mwanzo uwanjani Estadio do Dragao ambao ulikuwa umefurika hadi pomoni, kabla ya Mane kufungua ukurasa wa mabao kwa msaada wa mfumo wa VAR.

Liverpool sasa wana kibarua dhidi ya Barcelona katika nusu fainali.

Author: Bruce Amani