Liverpool yaichapa 4-0 Arsenal EPL

Liverpool imeibuka kidedea mbele ya Arsenal na kuhitimisha ushindi wa mechi 10 mfululizo kwao baada ya kuvuna alama tatu wakiwa nyumbani katika dimba la Anfield.

Magoli ya Liverpool inayonolewa na kocha Jurgen Klopp yamefungwa na Sadio Mane, Mohamed Salah, Diogo Jota na Takumi Minamino huku nyota wa mchezo huo akiwa ni Trent Alexander Arnold beki wa kulia baada ya kutoa msaada wa goli mbili kwenye ushindi huo wa goli 4-0.

Ushindi huo unaifanya Liverpool kukwea mpaka nafasi ya pili nyuma ya vinara Chelsea wakati Arsenal wakibakia nafasi ya tano.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends