Liverpool yaichapa Arsenal 3-0 na kufufua matumaini ya kumaliza katika nne bora EPL

Liverpool imeichapa Arsenal bao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu nchini England uliopigwa dimba la Emirates, kijana wa Ureno Diogo Jota akiendeleza kasi ya kufumania nyavu.

Kufuatia Chelsea kupigwa kipigo cha aibu na kibonde West Bromwich Albion mapema Jumamosi, kunatengeneza mazingira ya Liverpool kuingia hatua ya nne bora kwenye msimamo wa EPL, sasa kocha Jurgen Klopp na vijana wake wanabakia alama mbili nyuma ya The Blues wa Thomas Tuchel.

Licha ya kutawala mchezo kwa muda mwingi, iliwachukua dakika ya 64 Liverpool kufunga goli la kwanza kupitia mchezaji aliyeingia kutokea benchi Diogo Jota akimalizia pasi ya Trent Alexander- Arnold.

Mohamed Salah nyota wa Misri aliingia kambani kabla ya Jota kufunga la tatu na kuhitimisha furaha kwa Jurgen Klopp ambaye msimu huu umekuwa mgumu kwake baada ya kutwaa taji la EPL msimu uliopita.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares