Liverpool yaipiga Chelsea kwa penalti na kubeba Super Cup

61

Liverpool imeshinda taji la Uefa Super Cup kwa mara ya nne katika historia ya klabu hiyo kwa penati 5 – 4 baada ya sare ya goli 2-2 katika dakika 120 ndani ya dimba la Istanbul leo Jumatano.

Mlinda mlango mpya wa Liverpool Adrian ameibuka kuwa shujaa wa mchezo baada ya kupangua penati iliyopigwa na kinda Tammy Abraham na kuisaidia The Reds kushinda taji hilo.

Chelsea waliongoza mtanange huo kwa goli la mshambuliaji Olivier Giroud kunako kipindi cha kwanza akipokea pasi ya upendo ya Pulisic kabla ya Sadio Mane kusawazisha na kufunga goli la kuongoza baada ya kazi nzuri ya Roberto Firmino aliyeingia kipindi cha pili.

Upande wa Chelsea goli la pili la kusawazisha limefungwa kwa penati na Jorginho baada ya Tammy Abraham kuangushwa kwenye 18.

Ushindi wa leo unakuja ikiwa ni siku 60 tu zimepita tangu kocha Jurgen Klopp kuiongoza Liverpool kutwaa taji lake la kwanza la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuifunga Tottenham 2-0 mchezo wa fainali..

HISTORIA MPYA KWA ADRIAN

Wiki mbili zilizopita kipa Adrian alikuwa hana timu ya kuchezea msimu ujao baada ya kuachwa na West Ham.

Hii ni kufuatia Simon Mignolet kuondoka klabuni Liverpool kujiunga na Club Brugge, Klopp akaona hana namna Alison majeruhi ndiyo akamuita Adrian ambaye ameisaidia klabu hiyo kutwaa taji la Uefa Super Cup.

Author: Bruce Amani