Liverpool yamuongeza Henderson mkataba mpaka 2025

Nahodha wa Liverpool Jordan Henderson amekubali kumwaga wino wa kuendelea kukitumikia kikosi hicho mpaka mwaka 2025.

Nahodha huyo mwenye umri wa miaka 31, amecheza mechi 394 tangia kusajiliwa kwake katika miaka 10 iliyopita, kandarasi ya miaka miwili ilikuwa imebakia.

Henderson ni mchezaji wa tano kuongeza mkataba mpya baada ya Trent Alexander-Arnold, Fabinho, Virgil van Dijk, Alison na Andy Robertson kuongeza mkataba mpya.

“Ni jambo la kipekee kuendelea kusalia hapa, safari yetu ya mafanikio inaendelea”.

Tangia kutua Anfield kutokea Sunderland mwaka 2011, Henderson ameshinda mataji matano moja wapo ni lile alizoshinda na kocha Kenny Dalglish Kombe la Ligi mwaka 2012.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares