Liverpool yaongeza mwanya wa pointi kileleni

Hii kasi ya Liverpool haikamatiki. Licha ya ubingwa wa EPL kutotabilika bado naendelea kuamini hao ndiyo mabingwa wapya wa EPL msimu huu 2019-20.

Leo Jumatano wameichapa West Ham goli 2-0 na kuvuna alama 19 zaidi ya timu iliyo nafasi ya pili Manchester City, wameshinda jumla ya mechi 41 tangu kampeni hii kuanza, nani wa kuwazuia vijana hawa wa Klopp.

Mohamed Salah na Alex Oxlade-Chamberlain ndiyo walioingia kwenye vitabu vya kumbukumbu kama wafungaji katika mtanange huo huku goli la Salah likifungwa kwa penati baada ya Divork Origi kuangushwa.

Matokeo yanawabakiza wagonga nyundo wa London na alama 17 juu yao kuna Fc Bournemouth mwenye alama 18 na Watford alama 19 tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga.

Akizungumzia nafasi ya ubingwa Klopp amesema “Ataendelea kupambana mpaka siku ya mwisho, hatuwezi kubweteka hivi sasa tunajua historia ya ligi hii, mashabiki kuanza kushangilia ni haki yao hatuwezi kuwazuia” Alisema Klopp ambaye kabla ya kuja Liverpool alitokea Borussia Dortmund ya Ujerumani.

Author: Bruce Amani