Liverpool yatoka nyuma na kuilaza Lyon

55

Liverpool imelazimika kutoka nyuma na kushinda dhidi ya Lyon 3-1, mchezo uliokamilisha maandalizi mabaya zaidi kuwai kutokea ndani ya timu hiyo msimu wa 2019/20.

Liverpool ilianza kufungwa goli la kwanza kupitia Memphis Depay kwa penati baada ya mlinda mlango Alisson kumwangusha Moussa Dembele dakika za mapema.

Moto wa Liverpool ulianza kuwaka kupitia kwa bingwa wa Copa America Roberto Firmino, kisha Joachim Andersen akijifunga na mwisho goli la kutamatisha ushindi wa Majogoo hao wa Anfield, likifungwa na Harry Wilson kwa shuti kali la umbali wa mita 25.

Ushindi wa leo unaipa nguvu Liverpool kuelekea mchezo wa Jumapili Agosti 4 dhidi ya Manchester City wa Ngao ya Jamii.

Umekuwa ni msimu mbovu zaidi kwa Liverpool baada ya kukubali kupoteza michezo minne dhidi ya Borussia Dortmund, Sevilla, Sporting Lisbon na Napoli.

Katika mchezo wa leo, wachezaji watatu waliokuwa bora msimu uliopita wameonekana katika kikosi hicho ambapo ni Mohammed Salah, Roberto Firmino na Alisson, hivyo amebakia Sadio Mane pekee amepewa mapumziko marefu zaidi kutokana na mashindano ya Afcon.

Author: Bruce Amani