Liverpool yaungana na Chelsea, Manchester City kutinga hatua ya 16 bora
Curtis Jones ametupia bao pekee kwenye ushindi wa Liverpool 1-0 dhidi ya Ajax likiwa ni bao lake la kwanza katika mashindano ya Uefa na kuisaidia timu yake kufuzu kuingia hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika kundi D.
Goli la Jones pengine waweza sema kipa wa Ajax Andre Onana aliamua kuwazawadia Liverpool kufuatia makosa binafsi ya mlinda mlango huyo raia wa Cameroon kutosevu krosi ya Neco Williams.