Liverpool yavuta kifaa kipya Anfield, yaleta beki wa kati Ben Davies

Klabu ya Liverpool imekamilisha uhamisho wa beki kitasa wa Preston North End Ben Davies na kujiunga na miamba hiyo ya soka nchini England Liverpool ambao pia ni mabingwa watetezi wa EPL.

Wakati huo huo kocha Jurgen Klopp amesema timu hiyo iko hatua ya nzuri kufanya uhamisho wa Ozan Kabak wa Schalke 04 ambaye ni raia wa Uturuki.

Ni kutokana na Hofu ya kuumia kwa ‘Kaka mkubwa’ Virgil van Dijk na Joel Gomez ambao wote kwa pamoja sio sehemu ya kikosi kwa msimu huu baada ya kupata majeruhi ya muda mrefu.

KWINGINEKO

West Bromwich Albion imekamilisha uhamisho wa kiungo wa Celta Vigo Okay Yokusluba na kiraka wa Arsenal Ainsley Maitland-Niles.

Newcastle wamesajili jina la kiungo wa zamani wa Arsenal Joe Willock kwa mkopo wakati ambao Newcastle United pia imepoteza mchezaji wake kwenda Galatasaray.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares