Loew kujadili na Hoeness uamuzi wa kuwatema nyota wa Bayern

Kocha wa Ujerumani Joachim Low anatarajiwa kukutana na rais wa Bayern Munich Uli Hoeness kujadili uamuzi wa kuwaondoa katika timu ya taifa wachezaji watatu nyota wa klabu hiyo.

“Tumepanga kukutana hivi karibunim” Hoeness aliliambia jarida la michezo la Bild nchini Ujerumani. Loew alitangaza hivi karibuni kuwa Jerome Boateng (30), Mats Hummels (30) na Thomas Mueller (29) hawatakuwa sehemu ya kikosi cha taifa wakati akikijenga upya kuelekea mashindano ya Euro 2020.

Aliwafahamisha wachezaji hao watatu muda mfupi kabla ya kuanza kwa msimu wa mechi za kimataifa na wakati Bayern kijiandaa kukabiliana na Liverpool katka hatua ya 16 za mwisho ya Champions League.

Bayern, kupitia mwenyekiti Karl-Heinz Rummenigge na mkurugenzi wa spoti Hasan Salihamidzic, walikubaliana na uamuzi huo wa Loew lakini wakapinga namna ambavyo ulifanyika. Ujerumani inacheza na Serbia Jumatano katika mechi ya kirafiki kabla ya kucheza nchini Uholanzi Jumapili mtanange wa kufuzu Euro 2020

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends