Logarusic amepewa mikoba ya kuinoa Zimbabwe

Shirikisho la soka nchini Zimbabwe limemteua Zdravko Logarusic raia wa Croatia, kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya The Brave Warriors.

Logarusic, mwenye umri wa miaka 54 amechukua nafasi hiyi baada ya kutokea nchini Sudan, alikimaliza mkataba wake mwezi Desemba mwaka uliopita.

Ametia saini mkataba wa miaka miwili na atasaidiwa na mzawa Joey Antipas, ambaye amekuwa akikaimu nafasi hiyo tangu Agosti mwaka uliopita.

Kazi kubwa iliyo mbele yake ni kuisaidia Zimbabwe kufuzu kucheza fainali ya mataifa binga barani Afrika mwaka 2021 nchini Cameroon na kombe la dunia nchini Qatar mwaka 2022.

Logarusic, ana uzoefu wa kufunza soka barani Afrika, amewahi kufunza soka ya Asante Kotoko , King Faisal Babes na Ashanti Gold kutoka Ghanam Interclube ya Angola, Gor Mahia na AFC Leopard ya Kenya na Simba ya Tanzania.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends