Lopetegui apinga La liga kuchezwa Marekani

Kocha wa Real Madrid Julen Lopetegui amekosoa mipango ya ligi ya Uhispania, La Liga ya kucheza na Marekani akisema kwamba inaondoa mazingira mazuri ya ushindani. Ligi hiyo, siku ya Jumanne iliomba idhini kutoka kwa shirikisho la soka la Uhispania, ya kuchezwa mechi ya Girona dhidi ya mabingwa wa La Liga, Barcelona mjini Miami ifikapo January 26.

“Siungi mkono kile kinachofanyika” alisema Lopetegui kwenye mkutano na waandishi wa habari. “Haina manufaa yoyote katika usawa wa mashindano. Timu zote zinatakiwa kucheza kwenye viwanja vilevile.” Madrid, ambao ni vinara wenza na Barcelona, inaendeleza kampeni zake itakapokutana na Athletic Bilbao Jumamosi hii, ikiangazia ushindi wa nne mfululizo, wakiwa na lengo la kuendeleza rekodi kwa asilimia 100.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends