Luis Jose Miquissone mali halali ya Al Ahly

Matajiri wa Afrika Kaskazini Klabu ya Al Ahly leo Agosti 26 imemtambulisha Luis Miquissone kuwa winga wao kuanzia msimu mpya wa mashindano ya 2021/22.

Nyota huyo raia wa Msumbiji alikuwa anakipiga kunako klabu ya Simba kwa sasa ni rasmi atakuwa mali ya Waarabu hao wa Misri baada ya kukamilisha utaratibu mzima wa kupata saini yake.

Kwa msimu uliopita wa 2020/21 ndani ya Ligi Kuu Bara alihusika katika mabao 19 kati ya 78 ndani ya Simba. Alifunga 9 na kutoa jumla ya paso 10

Hali kadhalika, kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, dimba la Mkapa aliwatungua Al Ahly bonge moja ya bao akiwa nje ya 18 kwa pasi ya mshikaji wake Clatous Chama ambaye naye amesaini dili la miaka mitatu RS Berkane ya Morocco. Unajua

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares