Luiz apewa mkono wa kwakheri Arsenal

118

Beki wa kati wa Brazil na klabu ya Arsenal David Luiz ataachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 34, alikutana na Uongozi wa klabu hiyo Ijumaa kwa ajili ya kuzungumza juu ya hatima yake ikiwa miaka miwili imesalia kuhitimisha kabumbu ndani ya Emirates.
Luiz amecheza jumla ya mechi 30 katika mashindano yote msimu huu lakini The Gunners wanahitaji damu changa katika msimu ujao 2021/22.
Kitasa huyo wa zamani wa Chelsea na Paris St-Germain, alijiunga na Arsenal mwaka 2019 akitokea Chelsea kwa ada ya pauni milioni 8

Author: Bruce Amani