Lukaku afunga goli mbili wakati Inter Milan ikishinda mbele ya Borrusia Monchengladbach 3-2

120

Romelu Lukaku aliingia nyavuni mara mbili kwa Inter Milan katika ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Borrusia Monchengladbach na kutengeneza mazingira mazuri ya kufuzu kuingia hatua ya mtoano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya. Borrusia Monchengladbach ilikuwa na nafasi ya kuwa vinara wa kundi B lakini walijikuta wakipoteza mchezo huo dhidi ya Inter Milan iliyoonekana kuwa bora.

Hata kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika Alassane Plea alifuta bao la mapema la Matteo Darmian. Lukaku akafunga mbili na Plea akaongeza la pili na mtanange kumalizika 3-2.

Kwingineko, Real Madrid wamekutana na kichapo cha goli 2-0 dhidi ya Shakhtar Donetsk mapema Jumanne na kufifisha matumaini ya kufuzu michuano hiyo hatua ya mtoano.

Author: Asifiwe Mbembela