Lukaku arejea kikosini Chelsea

Mshambuliaji wa Chelsea Romelu Lukaku anaweza kurejea uwanjani baada ya kuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki tatu akiuguza majeruhi aliyoyapata kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Novemba 2 dhidi ya Malmo.

Lukaku anaweza kuanza au kuanzia bechi kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Juventus mchezo wa hatua ya makundi, kundi H utakaopigwa dimba la Stamford Bridge Leo Jumanne Novemba 23.

Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel alisema Lukaku “anaonekana yuko sawa” alisema hayo baada mchezo wa Ligi Kuu England uliopigwa wikiendi iliyopita dhidi ya Leicester City.

Chelsea wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi H, alama tatu pungufu ya zile za vinara Juventus, hata hivyo wanahitaji alama moja kwenye mechi mbili zilizosalia kufuzu hatua ya 16 bora.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends