Lukaku awapa ushindi Ubeligiji mbele ya Croatia

Romelu Lukaku ameendelea kuwa katika kiwango bora kwenye mechi za maandalizi ya michuano ya Euro 2020 baada ya kuisaidia timu yake ya Ubeligiji kuitandika bao 1-0 Croatia katika mchezo wa kupasha misuli uliopigwa Jana Jumapili.
Mshambuliaji huyo wa klabu ya Inter Milan alifunga bao pekee kunako dakika ya 38 lililodumu mpaka dakika tisini akimalizia mpira wa Jason Denayer.
Ubeligiji watafungua pazia la Euro 2020 kwa kucheza na Urusi Juni 12 kabla ya kukutana na Denmark Juni 17 na kumalizia mechi na Finland Juni 21.
Habari njema kwa Ubeligiji ni kuwa kiungo mshambuliaji wa Manchester City Kevin de Bruyne atajiunga na timu hiyo Leo Jumatatu baada ya kuimarika kutoka kwenye majeruhi yake aliyoyapata kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Chelsea.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares