Lukaku, Sanchez waipa ushindi Inter Milan dhidi ya Torino

192

Staa wa zamani wa FC Barcelona, Arsenal na Manchester United Alexis Sanchez na Romelu Lukaku wote wameisadia timu ya Inter Milan kupata matokeo chanya wakitokea nyuma kwa goli 2-0 dhidi ya Torino.

Fowadi wa zamani wa West Ham United Simone Zaza aliitanguliza Torino kabla ya Cristian Ansaldi kufunga goli la pili kwa tuta dakika ya 62.

Inter walisawazisha ndani ya dakika tano pekee. Kiujumla Sanchez, Lukaku na Lautaro Martinez wameipa ushindi Inter matokeo muhimu ambayo yanaifanya kukamata nafasi ya tano alama tatu nyuma ya vinara wa Ligi Sassuolo.

Author: Asifiwe Mbembela