Lukaku wa Inter Milan fundisho huru nyakati ngumu

Sio muda sana pale dunia na macho yangu yalitaka kuamini Lukaku si kitu. Si akiwa Chelsea wala Manchester United alionekana strika wa ajabu. Kila mmoja aliona ni mzigo kuwa naye kwenye timu.

Gia ili ‘lose’ Chelsea, ikadaka kwa mbali Everton, ikatema tena Manchester United kabla ya kushika vyema Inter Milan.

Lukaku hakuwai kuwa tegemeo Chelsea wala Manchester United, bila shaka presha ya matokeo ya vilabu hivyo ilikuwa inamuadhibu.

Angalau akiwa Everton, Bolingoli Lukaku alikuwa kwenye fomu nzuri kama mshambuliaji, ndiyo sababu Man United walikuwa radhi kutoa kitita kirefu cha fedha kumfanyia uhamisho na kutua viunga vya Old Trafford. Bila shaka aliondoka akiwa hana hamu ya kurudi tena klabuni hapo.

Sasa yuko Inter Milan, ni Romelu Lukaku mpya kabisa chini ya Antonio Conte, kila gia anayopiga kwa sasa inashika na kumpa kasi maradufu mithili ya swala aliyekoswa na Simba.

Asipofunga, anaasisti, na asipo asisti anacheza vyema – mambo ambayo yalikuwa nadura kuyaona ndani ya uzi wa The Blues, Mashetani Wekundu wala West Bromwich Albion na Everton.

Wikiendi iliyopita, alikuwa mchezaji wa pili Seria A kufunga goli 20 au zaidi kwa misimu mwili mfululizo. Baada ya mechi ya leo Jumatano amefikisha bao 21 na asisti 9 sawa sawa na mchango wa goli 30 kwenye mechi 28.

Bila shaka, akiangalia wakati wa nyuma alivyokuwa anapata shida kuamini, hatamani ijirudie hali ile.

Lukaku anatupa funzo kuwa katika maisha, sio lazima utusue maisha kwa elimu (kuajiriwa), unaweza tusua kwa kufanya jambo lolote lile kama kilimo ukafanikiwa ili mradi kuwepo kwa juhudi na nidhamu.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares