Lyon yaipa PSG kichapo cha kwanza cha msimu katika ligi

171

Wengi walikuwa wakijiuliza nani atakayeivuruga rekodi ya miamba wa kandanda Ufaransa Paris Saint Germain. Jibu lilipatikana Jumapili wakati vinara hao wa ligi kuu ya Ufaransa kupata kipigo cha kwanza cha msimu baada ya penalty ya kipindi cha pili ya Nabil Fekir kuwapa Lyon ushindi.

Vijana hao wa kocha Thomas Tuchel walichukua uongozi kupitia bao la Angel Di Maria, aliyesukuma wavuni bao katika dakika ya saba. Moussa Dembele alisawazisha kabla ya Fekir kuhakiisha kuwa PSG wanalala kwa mara ya kwanza msimu huu kwenye ligi.

Licha ya kichapo hicho, PSG bado wanaongoza kileleni na mwanya wa pointi 10 dhidi ya nambari  mbili Lille na faida ya mechi mbili zaidi za kucheza. Lyon wako nyuma katika nafasi ya tatu.

Author: Bruce Amani