Maafisa 6 wakuu wa Barcelona wajiuzulu

45

Majanga bado yanaiandama Barcelona, ambapo leo viongozi sita ndani ya klabu hiyo wamejiuzulu na kuandika barua ya pamoja kwenda kwa Rais wa klabu hiyo kuwa hawapendi namna anavyoiongoza klabu.

Katika barua ya pamoja wote sita, wamesema wanashangaa namna Rais Josep Maria Bartomeu anavyoyashughulikia matatizo mbalimbali kama virusi vya Corona hivi sasa.

Viongozi wamekosoa pia namna ambavyo klabu ilifikia tamati ya skando ya mwezi wa pili ambapo Barca ilikumbwa na kashfa ambayo Rais aliiteea kwa ajili ya kulinda picha yake. Kashfa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii iliwataja wachezaji kama Lionel Messi, Gerrard Pique na Xavi kuwa kwenye mgogoro baina ya pande mbili.

Pia wameongeza kuwa ili kuwa na manufaa kwa siku za usoni ndani ya Barcelona viongozi hao sita wamependekeza kufanyika kwa uchaguzi wa Rais.

Majina ya wajumbe hao ni Emili Rousaud, Enrique Tombas (Wote makamu wa Rais) – Wakurugenzi wanne Silvio Elias, Josep Pont, Jordi Calsamiglia na Maria Teixidor.

“Hatuwezi kuendelea kuwepo hapa katika kipindi hiki ambacho klabu imeshindwa kutatua changamoto za baadae baada ya kumalizika kwa majanga tofauti tofauti hasa baada ya kuisha kwa COVID-19”. Waliandika wajumbe hao katika barua ya pamoja.

“Tumetoka madarakani kuonyesha kuwa hatukukubaliana na ile video iliyosambaa kwenye mtandao wa kijamii unaofahamika kama Barcagate”.

Barca wamejibu barua hiyo na wamesema wamepokea barua kutoka kwa wajumbe hao wa bodi ya timu lakini wataendelea kuongozwa na Rais wa sasa Bwana Bartomeu.

Pia klabu imekanusha kuhusu kashfa ya mtandao wa kijamii.

Katika kipindi hiki cha Corona wachezaji na viongozi wa Barcelona wamekubaliana kukatwa asilimia 70 ya mishahara yao kwenda kwa wafanya kazi wasio wanamichezo wanaotakiwa kulipwa mishahara yao kipindi hiki.

Bodi, wajumbe na timu ya kikaku ya Barca wamekubali mishahara yao kukatwa pia asilimia sawa na wachezaji.

Author: Bruce Amani