Maajabu ya Madagascar kuendelea leo mbele ya Tunisia?

68
Timu ya taifa ya Madagascar inaingia uwanjani leo Julai 11 kujaribu kama bahati ya kufanya vizuri itaendelea dhidi ya Tunisia katika mchezo wa robo fainali wa mashindano ya Afcon 2019 mchezo utakaopigwa majira ya 4 usiku.
Ikiwa ndio mara ya kwanza kushiriki mashindano ya Afcon katika historia ya Taifa hilo Madagascar inaingia dimbani leo baada ya kuiondosha Congo hatua ya 16 bora kwa mikwaju ya penati baada ya sare ya 2-2. Timi hii ina ari kubwa ikichagizwa na uwepo wa Rais wao.
Upande wa Tunisia wanaingia kwenye mchezo kwa kujiamini baada ya kuifunga Ghana 16 bora kwa penati baada ya sare ya goli 1-1 kunako dakika 120. Huu utakuwa mchezo wa mwisho wa hatua ya robo fainali kwa maana robo fainali inafungwa leo Alhamis Julai 11 na kuingia hatua ya nusu fainali.

Author: Bruce Amani