Maambukizi mapya ya corona yaipata klabu ya Dresden ya Ujerumani, sasa waingia karantini kwa mara nyingine

Timu ya ligi daraja la pili Ujerumani (Bundesliga 2) Dynamo Dresden imethibitisha kupata maambukizi mpya ya virusi vya Corona kwa watu wawili wa klabu hiyo, maambukizi yaliotokea kipindi ambacho klabu hiyo imejitenga tangu Mei 9 baada wachezaji wawili kukutwa na virusi hivyo.

Taarifa kutoka ndani ya Dresden imesema mchezaji mmoja, na mmoja wa makocha wa timu hiyo wamekuwa na virusi hivyo baada ya vipimo vya Covid-19.

Maambukizi hayo mapya yana maanisha klabu hiyo itaendelea kukaa karantini kwa siku nyingine 14 ingawa timu itaendelea na mazoezi yake siku ya Jumamosi.

“Idara ya afya ya Dresden imefanya kazi kwa wajibu mkubwa kwa kuiweka timu hiyo karantini kwa wiki nyingine mbili lakini wachezaji watokee nyumbani na sio kambini tena, utaratibu huu utafutiliaji mbali mnyororo wa kuambukizana katika timu”, alisema Daktari wa timu hiyo Onays Al-Sadi.

Bundesliga na Bundesliga 2 zote zilianza kutimua vumbi tena baada ya kusimama kwa zaidi ya siku 70 Jumamosi iliyopita Mei 16 ambapo ziliandikisha historia ya kuwa ligi ya kwanza kubwa kurejea, lakini pamoja na kurejea kwake bado Dresden hawakucheza mchezo wao kutokana na wachezaji wa timu hiyo kuwa karantini kwa wiki mbili

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends