Maamuzi magumu sasa lazima yachukuliwe kuinusu EPL

44

Vilabu nchini Uingereza vipo katika meza ya makubaliano ya kufanya maamuzi magumu kipindi hiki ambacho kuna virusi vya Corona hasa namna ya kujikimu kiuchumi.

Hayo yamesemwa na viongozi wa EPL, EFL na PFA katika kikao cha dharura kilichoikutanisha mihimili hiyo mitatu katika kujadili anguko ambalo linaweza kutokea kwa vilabu kutokana na uwepo wa COVID-19 ambapo wameendelea kutoa mishahara bila kazi kwa wafanya kazi wake.

Itakumbukwa michezo yote ilisimamishwa angalau mpaka Aprili 30 kukiwa na uwezekano wa kusogeza mbele zaidi endapo maambukizi yatakuwa makubwa au hakutakuwa salama.

EPL, EFL na PFA wametoa kauli rasmi ambayo ilisomeka kuwa “Tuna amini kila mmoja wetu ameathirika na virusi hivi kwa namna moja”.

“Tumekubaliana kuwa tufanye kazi kwa kushirikiana na kupata jibu la tatizo kwa pamoja”.

Vikao vingine vimepagwa kufanyika kuanzia wiki lijalo kujadili mpango mpya wa kukabiliana na wakati huu mgumu ambao haukuwai kuikumba ligi hiyo, klabu, wachezaji, viongozi wa timu wala mashabiki”.

Baadhi ya mambo yanayoibua hisia kuwa huenda yakajadiliwa ni pamoja katika vikao vijavyo ni pamoja na kupunguza mishahara kwa wachezaji na viongozi wengine kwa ajili ya kwenda kuisaidia mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

Wachezaji wa Bayern Munich na Borrusia Dortmund wamekubaliana mishahara yao ikatwe ili pesa zisaidie kwenye vita na COVID-19.

Mpaka sasa haieleweki kama kweli Ligi Kuu ya England na EFL itamalizika kweli msimu, FA tayari wameshafuta ngazi zote za michezo nchini humo.

Zaidi ya timu ziko tayari kupingana na maamuzi ya FA kwani endapo ligi itafutwa hakutakuwa na timu kupanda daraja wala kushuka.

Author: Bruce Amani