Mabingwa watetezi Liverpool watupwa nje na Atletico Madrid

Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Liverpool wamevuliwa rasmi taji na kutolewa nje ya mashindano hayo baada ya kukubali kichapo cha jumla goli 4-2 dhidi ya timu ngumu ya Atletico Madrid hatua ya 16 bora.

Katika mtanange uliopigwa dimba la Anfield jana Jumatano Liverpool walitangulia kufunga goli dakika za mwishoni mwa kipindi cha kwanza likifungwa na Georginio Wijnaldum, goli lililodumu mpaka dakika tisini ambapo ziliongezwa dakika 30(muda wa ziada) kupata mshindi ikumbukwe mechi ya raundi ya kwanza iliisha kwa Atletico kushinda goli moja.

Dakika 130 zitakumbukwa zaidi na Liverpool kwani wamejikuta wakiruhusu goli tatu huku makosa binafsi ya Andrian yakichangia kupoteza kwa aibu mbele ya mashabiki lukuki waliojitokeza kushuhudia mchezo huo.

Roberto Firmino aliipa Liverpool matumaini ya kusonga mbele baada ya kufunga goli la pili kabla ya Madrid hawajaamuka na kufunga goli za haraka kupitia kwa Marcos Llorente aliyefunga mbili sambamba na strika wa zamani wa Chelsea Alvaro Morata.

TAKWIMU

👉Inakuwa mara ya kwanza Liverpool inashindwa kuendelea hatua inayofuatia ya mashindano yanayohusisha mechi mbili(H & A) kama Uefa tangu Klopp aingie klabuni hapo, ameshinda mechi 10.

👉 Liverpool unakuwa mchezo wa kwanza katika mashindano ya Ulaya timu hiyo inapoteza nyumbani mara ya mwisho ilikuwa Oct 2014

👉 Atletico Madrid wamesonga mbele katika mechi tano kati ya sita ambazo mchezo wa kwanza waliongoza kwa ushindi.

👉 Liverpool wamepoteza raundi zote mbili za Uefa kwa mara ya kwanza tangu 2005-06 ambapo ilichapwa nje ndani ya Benfica.

👉Katika historia ya michuano ya Uefa haijawai kutokea goli nne kufungwa katika dakika za muda wa ziada (extra time) hii mechi ni ya kwanza.

👉Goli la Firmino dhidi ya Atletico limefuta ukame wa magoli kwa strika huyo katika dimba la Anfield ambapo alikuwa hajafunga katika michezo 20.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends