Madagascar ni moto wa kuotewa mbali katika Afcon

Madagascar walikuwa namba 190 kwenye viwango vya Fifa miaka mitano iliyopita lakini kinachoendelea kutokea Misri ni tofauti na namba hizo kwani sasa imepanda kwenye viwango vya Fifa.
Kwenye mchezo wa leo Jumapili imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya kwanza tangu taifa hilo kuanzishwa baada ya kuifunga DR Congo kwa penati ya goli 4-2 baada ya sare ya 2-2.
Madagascar ilipata goli la kuongoza kupitia kwa Ibrahim Amada kwa shuti kali kabla ya mshambuliaji Cedric Bakambu kusawazisha kwa mpira wa kichwa. Mpaka dakika 45 zinamalizika ilikuwa 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa faida ya Madagascar baada ya strika Faneva Andriatsima kufunga goli licha ya kusawazishwa tena na Chancel Mbemba kwenye dakika za nyongeza.
Mchezaji wa Everton na DR Congo Yannick Bolasie alikosa penati pamoja na mlinzi wa timu hiyo.
Madagascar wamekuwa bora kuanzia hatua ya makundi baada ya kuifunga Nigeria ambayo imetwaa taji la Afcon mara tatu, na Burundi.
Matokeo ya Madagascar kwenye Afcon 2019 yamewapa ugumu wachambuzi wengi wa soka kutokana na namna timu ambayo ni mpya lakini inafanya vyema na kuifunga timu ngumu kama Nigeria na Congo.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments