Madagascar yatoa onyo kwa Congo

Watu wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo leo Jumapili wanaelekeza macho yao katika mchezo wa hatua ya 16 bora wa mashindano ya Kimataifa Africa Afcon 2019 ambapo timu yao inaingia uwanjani kumenyana vikali na Madagascar mchezo utakaopigwa dimba la Alexandria kuanzia saa 1 usiku.

Congo wanaingia kwenye mchezo huo baada ya kufuzu kama timu iliyofanya vizuri kwa kuwa na wastani mzuri hasa baada ya kuipiga Zimbabwe kwa goli 4-0 huku Madagascar ikiwa timu kinara katika kundi lililo na bingwa mara tatu wa Afcon Nigeria.

Congo mwaka 2017 aliifunga Madagascar goli 8-2 katika michezo ya kufuzu Afcon kwa mikondo miwili.

Ikiwa chini ya Makocha wazawa Ibenge na Mwinyi Zahera Congo ilianza vibaya hatua ya makundi kwa kupoteza dhidi ya Uganda wakati Madagascar ikiwa bora tangu mchezo wa kwanza.

Afcon ya mwaka huu imekuwa na maajabu mengi ambapo mpaka sasa timu vigogo zimesha ondoshwa kwenye michuano hiyo Misri wenyeji, Cameroon,Morocco ni miongoni mwa timu zilizoaga mashindano hayo.

Mshindi wa mtanange wa huo atakutana na mshindi kati ya Algeria na Guinea hatua ya robo ya fainali za Afcon 2019 nchini Misri.

Author: Bruce Amani