Madrid chini ya ulinzi mkali kabla ya fainali ya Champions League

Uhispania imesema itaweka hatua kali kabisa za ulinzi kwa ajili ya fainali ya Jumamosi “yenye hatari ya kiusalama” ya Champions League mjini Madrid.

Mamlaka za Uhispania zimesema operesheni ya polisi inayojiandaa kwa ajili ya fainali kati ya Liverpool na Tottenham itakuwa kubwa kabisa kuwahi kushuhudiwa katika tukio la kandanda katika mji huo mku wa Uhispania.

Maafisa wanasema hatua hizo zitakuwa zaidi ya zilizochukuliwa katika fainali yam waka jana ya Kombe la Amerika Kusini Copa Libertadores kati ya mahasimu wa Argentina River Plate na Boca Juniors, mechi ambayo pia ilitajwa kuwa yenye hatari kubwa ya kiusalama

Zaidi ya polisi 4,700 watahusishwa katika operesheni ya Champions League, ambayo kwa mara ya kwanza itajumuisha ndege zisizoruka na rubani kufuatilia mienendo ya mashabiki.

Zaidi ya mashabiki 30,000 wa England wanatarajiwa kutizama fainali hiyo katika uwanja wa Wanda Metropolitano wenye uwezo wa kuwakaribisha watu 68,000

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends