Madrid yavuna ushindi na kukaa kileleni mwa La Liga

Ushindi mwembamba, mwendo wa kusuasua umeendelea kwa kocha Carlo Ancelotti wa Real Madrid, hii ni baada ya kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Real Betis katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga huku wakiendelea kuhusishwa kumsajili Kylian Mbappe.

Walikuwa wanaelekea kutoshana nguvu kwenye mechi hiyo kabla ya beki wa kulia Dani Carvajal kukwamisha mpira nyavuni kwa shuti akitumia vyema mpira wa krosi wa mshambuliaji wa Kifaransa Karim Benzema.

Benzema akiwa nje ya ubora wake alipoteza nafasi dakika za awali kabla ya Carvajal kufunga goli hilo ambalo ni kifuta jasho kwa kocha Carlo Ancelotti.

Licha ya ubovu wa Madrid katika mchezo huo, jaribio la karibu kupata goli kwa Betis lilitokea kufuatia mpira wa kutengwa uliopigwa na Nabil Fekir.

Real wako kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga wakiwa na alama saba sawa na Sevilla, Valencia na Mallorca.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares