Magadascar yatoka sare ya 2 – 2 na Guinea

Madagascar wamecheza kampeni yao kwa mara ya kwanza kabisa ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kutoka sare ya 2 – 2 dhidi ya wapinzani wa Kundi B Guinea mjini Alexandria.

Sory Kaba aliiweka Guinea kifua mbele baada ya dakika 34, lakini Madagascar wakajibu kwa kufunga mabao mawili katika dakika sita za kipindi cha pili kupitia Anicet Andrianantenaina na Charles Carolus Andriamahitsinoro.

Penalty ya Francois Kamano katika dakika ya 66 iliwapa Guinea pointi moja, baada ya  Romain Metanire kumwangusha Ibrahima Traore.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends