Majeruhi kumweka Philippe Coutinho miezi sita nje ya uwanja

92

Kiungo mshambuliaji wa Barcelona Philippe Coutinho atakuwa nje ya uwanja kwa miezi sita baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti. Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil, 28, alihitaji upasuaji baada ya kupata majeruhi hayo katika mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1 dhidi ya Eibar.

Coutinho, ambaye msimu uliopita alikitumikia kikosi cha Bayern Munich kwa mkopo, amecheza mechi 14 pekee msimu ndani ya Barcelona. Mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool anaungana na wachezaji wengine walio vitandani wakiuguza majeruhi yao kama kinda Ansu Fati na beki Gerard Pique.

Author: Asifiwe Mbembela