Majeruhi ya Neymar Jr yaipa tumbo joto Paris St-Germain

387

Klabu ya Paris St-Germain imesema vipimo vya majeraha ya staa wao Neymar Jr vimesogezwa mbele baada ya kuumia katika mchezo wa Ligue 1 dhidi ya Lyon.

Fowadi huyo raia wa Brazil alibebwa kwenye machela katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Ufaransa dhidi ya Lyon ambao ulimalizika kwa kipigo ambapo ilitajwa kuwa ni enka ya kushoto lakini kuhusu muda wa kukaa nje haijafahamika bado.

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo, Neymar atafanyiwa vipimo tena ndani ya masaa 48 yajayo. Licha ya vipimo hivyo kusogezwa mbele bado inaaminika kuwa majeruhi yake sio makubwa kiasi cha kukosa mechi za hatua ya 16 za Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya klabu yake ya zamani ya FC Barcelona.

Vilabu hivyo viwili vitachuana vikali tarehe za mwishoni mwa mwezi Februari, 2021. Neymar alijiunga na PSG kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 200 ambayo ilikuwa ni rekodi mwaka 2017.

Author: Bruce Amani