Majina 23 ya Burundi Swallows kwenda Afcon 2019

Timu ya Taifa ya Burundi chini ya Kocha Olivier Niyungeko imeweka bayana majina 23 ya kikosi kitakachoenda Misri katika Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 yanayotarajiwa kuanza Juni 21 huku Intamba m’Urugamba ikiwa ipo kundi B.

Kwenye kikosi hicho yupo mshambuliaji Saido Berahino na Laudit Mavugo ambao wamesakata kabumbu maeneo mbalimbali.

Kikosi kizima kipo hivi :-

WALINDA MLANGO

1 Jonathan Nahimana
2 Justin Ndikumana
3 MacArthur Arakaza

MABEKI

4 Frédéric Nsabiyumva
5 Moussa Omar
6 David Nshimirimana
7 Ngando Omar
8 Christophe Nduwarugira
9 Karim Nizigiyimana

VIUNGO

10 Pierrot Kwizera
11 Gaël Bigirimana
12 Gaël Duhayindavyi
13 Moustapha Francis
14 Enock Nsabumukama
15. Shassir Nahimana

WASHAMBULIAJI

 1. Fiston Abdoul-Razak
  17. Saido Berahino
  18. Mohamed Amissi
  19. Cedric Amisi
  20. Shabani Hussein
  21 . Kamsoba
  22. Laudit Mavugo
  23. Selemani Ndikumana

Burundi ni miongoni mwa mataifa manne kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na kati yatakayoenda kushiriki michuano hiyo sambamba na Tanzania, Kenya, na Uganda.

Intamba mUrugamba ipo kundi B pamoja na Madagascar, Guinea, na Nigeria. Mchezo wa kwanza kwenye Afcon utakuwa dhidi ya Nigeria Juni 22.

Author: Asifiwe Mbembela