Makambo awekwa kando Horoya, kicheko kwa Yanga

Klabu ya Horoya inayoshiriki Ligi Kuu Guinea imeachana na aliyekuwa mshambuliaji wake Heritier Makambo kwa kile kilichoelezwa kuwa ni baada ya makubaliano ya pande mbili.

 

Makambo alisajiliwa na Horoya kwa mkataba wa miaka mitatu na mpaka sasa alikuwa ameitumikia timu hiyo kwa misimu miwili tu akitokea Yanga kipindi cha kocha Mwinyi Zahera.

 

Kuvunjwa kwa mkataba huo ni taarifa nzuri kwa mabosi wa Yanga ambao inaelezwa wamekuwa wanahitaji mchezaji huyo arejee katika kikosi chao.

 

Ilielezwa Yanga walipeleka ombi la kuhitaji kumsajili mchezaji huyo lakini ilishindikana kutokana na mabosi wa Horoya kuhitaji pesa nyingi.

 

Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram ya klabu ya Horoya ulimshukuru Makambo kwa kuwa nae kwa misimu miwili mfululizo na kumtakia kila la kheri.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares