Makame aipa Yanga alama tatu dhidi ya Coastal Union

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Sc Abdulaziz Makame ameibeba timu hiyo akifunga bao pekee lilitoa alama tatu kwa Wanajagwani.

Makame akiwa katika kiwango bora akitimiza majukumu yake ndani ya uwanja kwenye nafasi ya kiungo alifanikiwa kutoa msaada wa kufunga katika kandanda iliyopigwa dimba la Uhuru dhidi ya Coastal Union ya Tanga Ligi Kuu.

Ukiwa ushindi wa kwanza kwa Yanga msimu ndani ya ligi Kuu, Makame alipachika mpira wavuni kwa kichwa akimalizia pasi ya Ali Ali aliyepokea mpira wa kona kutoka kwa Mrisho Ngasa.

Licha ya ushindi huo Yanga ilikosa nafasi nyingi sawa na michezo iliyopita na kupoteza, Ruvu Shooting(1-0), Zesco(2-1) na sare ya Polisi Tanzania(3-3).

Ushindi huo unaifanya Yanga ikusanye jumla ya pointi nne baada ya kucheza michezo mitatu msimu huu wa 2019/20.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares