Makapteni England wafanya kikao cha kukatwa mishahara

Manahodha wa vilabu vya Ligi Kuu ya England wamefanya kikao kujadili mpango wa kukatwa mishahara yao asilimia 30 ili fedha hizo zikatumiki kwenye mapambano dhidi ya virusi vya Corona.

Mchakato huo umeanzishwa na nahodha wa Liverpool Jordan Henderson kama sehemu ya chagizo la kutoa kwenye mapambano hayo.

Licha ya kikao hicho lakini wachezaji wote walipigiwa simu kwa ajili ya kuwataka mishahara yao kukatwa.

Nahodha wa Crystal Palace Andros Townsend amesema chagizo hilo utadhani lina walenga wachezaji pekee.

Katika kikao hicho kilichofanyika kwa njia ya simu, manahodha wamepanga kukubali kukatwa fedha ambazo zitaenda kusaidia waathirika wa COVID-19.

Mbali na makapteni, pia kuna mjadala wa umoja wa chama cha wachezaji kutaka kuchangia hela kwa ajili ya NHS.

Aidha, Mpaka sasa haijulikani ni kiasi gani ambacho kitachangishwa na vipi vilabu vitachangishana pia au la.

Author: Bruce Amani