Makosa ya kipa Leno yaizawadia Everton nyumbani kwa Arsenal

336

Goli la kujifunga la mlinda mlango wa Arsenal Bernd Leno dakika za lala salama limewapa alama tatu Everton na kuendelea kufuta matumaini ya Washika Mtutu wa London kushiriki michuano ya Ulaya msimu ujao 2021/22.

Arsenal wanapokea matokeo hayo kipindi ambacho, zaidi ya mashabiki 1,000 wamekuwa wakiandamana nje ya uwanja wa Emirates kushinikiza uongozi wa juu wa timu hiyo kujiondoa akiwemo Stan Kroenke baada ya kukubali kujiunga na Ligi mpya ya European Super League.

Goli hilo limetokea baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Richarlison kujaribu kupiga pasi kuelekea golini hata hivyo mpira ulipoteza uelekeo na kwenda golini wakati Leno akiwa kwenye jitihada za kuushika ulimpita mikononi na kutinga kambani.

Mpaka dakika ya 90, mbali na kosa kosa za hapa na pale kwa timu zote mbili, kitambaa kilikuwa hakitoshi kwa Arsenal kuondoka na pointi angalau moja.

Everton wanafikisha pointi 52 wakati Arsenal 46 kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini England takribani michezo sita imebakia.

Author: Bruce Amani