Makosa ya Waamuzi Yalazimisha Matumizi ya VAR

59

Rais wa Shirikisho la Kandanda Duniani Fifa Gianni Infantino amesema mechi zote za mtoano za kufuzu Kombe la Dunia Qatar 2022 zitachezwa kukiwa na usaidizi wa refarii wa video (VAR).

Infantino amesema hayo baada ya kufika Doha Qatar ambako fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022 zitafanyika kwa ajili ya kuangalia maandalizi ya fainali hizo ambazo zitachezwa mwishoni mwa mwaka huo.

Lakini pia ameongeza kuwa hata michezo ya Afrika ya mtoano pia itachezwa kwa kutumia usaidizi wa refarii kuyafanya maamuzi kuwa sahihi ili kupunguza malalamiko kama ambayo Afrika Kusini waliyatoa dhidi ya Ghana.

“Tunatakiwa kutumia VAR kupunguza lawama na kuwasaidia waamuzi kuchukua maamuzi sahihi, kwa sababu inaonekana ni vigumu kufanya maamuzi pekee yako”.

Kwingineko, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika CAF Motsepe amesema wanaendelea na mpango wa kuona kunaanzishwa mashindano mapya ya African Super League ambayo ameyataja kuwa yataviongezea thamani vilabu.

Author: Bruce Amani