Man City imani juu yao mbele ya Borussia Monchengladbach kwenye Ligi ya Mabingwa

Kiungo mshambuliaji wa Manchester City Ilkay Gundogan amesema kutolewa kwao mapema kwenye hatua za mwanzoni katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita kunawafanya kuwa makini katika michezo ya sasa.

Kesho Jumatano vinara hao wa EPL watakuwa na kibarua kizito mbele ya timu kutoka Ujerumani Bundesliga ya Borussia Monchengladbach hatua ya 16 bora, mtanange utapigwa Budapest Hungary.

City waliichapa Real Madrid goli 3-1 katika hatua kama hii msimu uliopita lakini waliondolewa na Lyon ya Ufaransa kwenye mechi moja ya robo fainali mjini Lisbon.

“Hatuwezi kusahau, tuliumia ni lazima tuwe makini kuepuka makosa kama yale” alisema Gundogan ambaue yuko kwenye ubora mkubwa sana msimu huu.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares