Man City wapata majanga mapya

Mlinzi wa Manchester City John Stones atakuwa nje ya uwanja kwa wiki tano mpaka sita akitumikia majeraha ya misuli aliyoyapata leo mazoezini wakijiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Stones amepata majeraha hayo akiwa Ukraine ambapo kesho City itapepetana na Shakhtar Donetsk hatua ya makundi ukiwa mchezo wa kwanza 2019/20.
Huo unakuwa mtihani mwingine kwa kocha Pep ambaye anamkosa pia Aymeric Laporte mpaka mwezi Januari ambaye yupo nje kwa majeruhi pia. Chaguo pekee kwa kocha huyo ni mlinzi wa kati Nicolas Otamendi.
Huo ni mtihani kwani hivi sasa City wanaenda katika kipindi cha michuano mingi ama ratiba ya mechi mfululizo kuanzia Uefa, Epl, na Carabao Cup.
Stones, 25, mlinzi wa England atakosa zaidi ya mechi 8 za Ligi, na mechi za Kombe la Carabao.
“Kwa mimi kama Mwalimu ni changamoto kubwa kweli kweli,” alisema Pep baada ya tukio la kuumia kwa mlinzi Stones ambaye amekuwa na majeraha ya mara kwa mara.
City watakutana na Shakhtar kesho Jumatano kufuatiwa na Watford Jumamosi, kabla ya kuivaa Preston Deepdale raundi ya tatu ya kombe la EFL.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends