Man City yaendeleza presha kwa Chelsea, Liverpool

Manchester City imeshinda goli 4-1 dhidi ya wenyeji Brighton katika mchezo wa Ligi Kuu England ambao umepigwa Leo Jumamosi Octoba 23 huku kijana Phil Foden akifunga bao mbili.

Kikosi cha kocha Pep Guardiola kimefunga goli tatu za haraka ndani ya dakika 45 za kwanza kabla ya muda wa jioni kufunga mahesabu, kupitia kwa Ilkay Gundogan, Bernardo Silva, na Riyard Mahrez akifunga dakika za jioni kabisa.

Ungwe ya pili Brighton waliibuka na kuongeza mashambulizi ambapo kipa wa Man City Ederson alilazimila kufanya sevu nzuri na kubwa kabla ya kuruhusu bao la Enock Mwepu.

Msimu uliopita, Brighton walitoka nyuma kwa goli mbili na kushinda dhidi ya Man City lakini msimu huu maji yakazidi unga moja kwa moja.

Matokeo hayo yanaifanya Manchester City kuwa nafasi ya pili nyuma ya kinara Chelsea katika msimamo wa Ligi Kuu England kabla ya Liverpool kuwa ugenini kwa Manchester United.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends