Man City yafungiwa kucheza Ulaya misimu miwili

56

Manchester City wamepigwa marufuku kushiriki mashindano ya Ulaya kwa misimu miwili ijayo baada ya kupatikana na hatia ya kukiuka kanuni za Uefa za leseni na usawa wa kifedha na mapato.

Mabingwa hao watetezi wa Premier League pia wametozwa faini ya euro milioni 30. Uamuzi huo unaweza kupingwa katika Mahakama ya Usuluhishi wa mizozo Michezoni.

Manchester City wamesema wamesikitishwa lakini hawajashangazwa na uamuzi huo wanaosema ni wa kibaguzi na kuwa watakata rufaa.

Jopo huru la kijaji kutoka Shirika la Udhibiti wa Maswala ya Kifedha katik Vilabu limesema City ilivunja sheria kwa kudanganya mapato yao ya udhamini katika akaunti zao na taarifa zilizowasilishwa kwa Uefa kati ya 2012 na 2016 likiongeza kuwa klabu hiyo ilishindwa kutoa ushirikiano katika uchunguzi.

Author: Bruce Amani