Man City Yaichapa 3-1 Leicester City

69

Erling Haaland amefunga mabao mawili kwenye ushindi wa 3-1 walioupata Manchester City dhidi ya Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu England mtanange uliopigwa dimba la Etihad Jumamosi.

Mabao hayo yanamfanya Haaland kufikisha bao 47 kwenye mechi 40 ambazo amecheza kwenye mashindano yote msimu huu.

Bao lingine la Manchester City ambayo imepunguza pengo dhidi ya timu kinara Arsenal kufikia pointi tatu limefungwa na mlinzi wa kati wa England John Stones.

Hata hivyo, Arsenal wanaweza kurudisha pengo la pointi mpaka sita endapo watashinda kwa West Ham United Jumapili.

Bao la kufutia machozi kwa vijana wa Leicester City ambao walimfuta ukocha Brendan Rodgers limefungwa na mchezaji wa zamani wa Man City Kelechi Iheanacho.

Author: Bruce Amani