Man City Yaichapa Bayern, Kukutana na Real Madrid Nusu Fainali

158

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England Manchester City wamefuzu kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa kufuatia kuibuka na ushindi wa jumla wa mabao 4-1 dhidi ya Bayern Munich ambapo kwenye raundi ya pili ya robo fainali wametoa sare ya bao 1-1 baada ya ushindi kwa goli 3-0 walioupata kwenye mkondo wa kwanza uliochezwa dimba la Etihad.

Kwenye mkondo wa pili, Bayern walilazimika kushinda angalau kwa bao tatu bila jibu lakini haikuwa hivyo kwani bao la Erling Braut Haaland kwenye kipindi cha pili liliongeza mlima wa kupanda kabla ya bao la penati la Joshua Kimmich kuwa kama kifuta jasho dakika za lala salama.

Kwa matokeo hayo, Manchester City imetinga nusu fainali ambapo itacheza na Real Madrid ambayo iliitoa Chelsea kwa jumla ya mabao 4-0 kwenye mechi mbili za raundi ya kwanza na ya pili.

Author: Bruce Amani